Wazazi na walezi waliohudhuria kwenye mahafali ya Tano ya wahitimu waliomaliza mafunzo mbalimbali ya ufundi na Elimu ya mifugo wamefurahishwa na maonyesho ya vitendo yaliyoandaliwa na wahitimu hao.
Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Mto wa Mbu kimehitimisha wanachuo katika fani ya Umeme wa majumba, umeme wa magari, ufundi wa magari, mapishi na hotelia, na pia fani ya Elimu ya mifugo.
Mkuu wa Chuo akiongelea mafunzo yatolewayo hapo kwa mwaka wa masomo 2017 ni pamoja na ushonaji ambayo ni fani mpya kwa chuo hicho.
Wengi wa wahitimu walifurahia namna ambayo uongozi, wakufunzi na watumishi wote kwa ujumla wanavyowatunza na kuwafundisha na kuomba juhudi hizi ziendelee.
Tutaendelea kufuatilia kwa karibu chuo hiki kujua nini hasa kinafanya kipate sifa hizi.